Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mhu 10

10
Maoni Mengine
1Mainzi mafu huvundisha marhamu ya mwuza marashi;
Kadhalika upumbavu haba ni mzito kuliko hekima na heshima.
2 # Mt 6:33; Kol 3:1 Moyo wake mwenye hekima upo upande wa kuume;
Bali moyo wake mpumbavu upo mkono wa kushoto.
3 # Mit 13:16 Naam, huyo mpumbavu tena, aendapo njiani, hupungukiwa na fahamu zake; hata humwambia kila mtu ya kuwa yeye ni mpumbavu.
4 # Mhu 8:3; 1 Sam 25:24; Mit 25:15 Roho yake mtawala ikiinuka kinyume chako,
Usiondoke mara mahali pako ulipo;
Kwa maana roho ya upole hutuliza machukizo yaliyo makubwa.
5Liko baa nililoliona chini ya jua, nalo ni kama kosa litokalo kwake yeye atawalaye; 6ya kuwa upumbavu huwekwa mahali pa juu sana, nao wakwasi hukaa mahali pa chini. 7#Mit 19:10Mimi nimeona watumwa wamepanda farasi, na wakuu wakienda kwa miguu juu ya nchi kama watumwa.
8 # Zab 7:15; Mit 26:27 Mwenye kuchimba shimo atatumbukia ndani yake;
Na yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma.
9Mwenye kuchonga mawe ataumizwa kwayo;
Naye apasuaye miti huona hatari katika hiyo.
10Iwapo chuma hakipati, wala mtu hakinoi;
Ndipo hana budi kutumia nguvu zaidi. Walakini yafaa kutumia hekima, na kufanikiwa.
11 # Yer 8:17 Nyoka akiuma asijatumbuizwa,
Basi hakuna faida ya mtumbuizi.
12Maneno ya kinywa chake mwenye hekima yana neema;
Bali midomo ya mpumbavu itammeza nafsi yake.
13Mwanzo wa maneno ya kinywa chake ni upuuzi; na mwisho wa usemi wake ni wazimu wenye hatari. 14#Yak 4:14Tena, upumbavu huongeza maneno; lakini mwanadamu hajui yatakayokuwako; nayo yatakayokuwa baada yake, ni nani awezaye kumweleza?
15Kazi yao wapumbavu huwachosha kila mmoja,
Maana hajui hata njia ya kuuendea mji.
16 # Isa 3:4 Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana,
Na wakuu wako hula asubuhi!
17 # Mit 31:4 Heri kwako, nchi, mfalme wako akiwa mtoto wa watu,
Na wakuu wako hula wakati ufaao, Ili makusudi wapate nguvu, wala si kwa ajili ya ulevi.
18Kwa sababu ya uvivu paa hunepa;
Na kwa utepetevu wa mikono nyumba huvuja.
19Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko,
Na divai huyafurahisha maisha; Na fedha huleta jawabu la mambo yote.
20 # Kut 22:28 Usimlaani mfalme, la, hata katika wazo lako;
Wala usiwalaani wakwasi chumbani mwako;
Kwa kuwa ndege wa anga ataichukua sauti,
Na mwenye mabawa ataitoa habari.

Iliyochaguliwa sasa

Mhu 10: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia