Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Kor 3:12-18

2 Kor 3:12-18 SUV

Basi, kwa kuwa mna taraja la namna hii, twatumia ujasiri mwingi; nasi si kama Musa alivyotia utaji juu ya uso wake, ili kwamba Waisraeli wasitazame sana mwisho wa ile iliyokuwa ikibatilika; ila fikira zao zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo hivi, wakati lisomwapo Agano la Kale, utaji uo huo wakaa; yaani, haikufunuliwa kwamba huondolewa katika Kristo; ila hata leo, torati ya Musa isomwapo, utaji huikalia mioyo yao. Lakini wakati wo wote watakapomgeukia Bwana, ule utaji huondolewa. Basi “Bwana” ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru. Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.

Soma 2 Kor 3

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na 2 Kor 3:12-18