Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Wakorintho 3:12-18

2 Wakorintho 3:12-18 NEN

Kwa hiyo, kwa kuwa tunalo tumaini hili, tuna ujasiri sana. Sisi si kama Mose, ambaye ilimpasa kuweka utaji ili kufunika uso wake ili Waisraeli wasiuone ule mngʼao uliokuwa juu yake hadi ulipofifia na hatimaye kutoweka. Lakini akili zao zilipumbazwa, kwa maana mpaka leo utaji ule ule hufunika wakati Agano la Kale linasomwa. Huo utaji haujaondolewa, kwa maana ni katika Kristo peke yake unaondolewa. Hata leo Sheria ya Mose inaposomwa, utaji hufunika mioyo yao. Lakini wakati wowote mtu anapomgeukia Bwana, utaji unaondolewa. Basi Bwana ndiye Roho. Mahali alipo Roho wa Bwana hapo pana uhuru. Nasi sote, tukiwa na nyuso zisizotiwa utaji tunadhihirisha utukufu wa Bwana, kama kwenye kioo. Nasi tunabadilishwa ili tufanane naye, toka utukufu hadi utukufu mkuu zaidi, utokao kwa Bwana, ambaye ndiye Roho.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na 2 Wakorintho 3:12-18