Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Nya 13

13
Abiya Atawala Yuda
1 # 1 Fal 15:1 Katika mwaka wa kumi na nane wa mfalme Yeroboamu, akaanza Abiya kutawala juu ya Yuda. 2#2 Nya 11:20Miaka mitatu akatawala huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Maaka binti Urieli wa Gibea. Kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu. 3Abiya akapanga vita mwenye jeshi la watu hodari wa vita, watu wateule mia nne elfu; naye Yeroboamu akapanga vita juu yake mwenye watu wateule mia nane elfu, waliokuwa waume mashujaa. 4#Yos 18:22Basi Abiya akasimama juu ya kilima cha Semaraimu, kilichoko milimani mwa Efraimu, akasema, Nisikieni, enyi Yeroboamu na Israeli wote; 5#Amu 11:21-24; 1 Sam 16:12,13; 2 Sam 7:12-16; Zab 89:20; Lk 1:31-33; Hes 18:19je! Haikuwapasa kujua ya kwamba BWANA, Mungu wa Israeli, alimpa Daudi ufalme juu ya Israeli milele, yeye na wanawe kwa agano la chumvi? 6#1 Fal 11:26; 12:20,27; 2 Nya 10:19Lakini Yeroboamu mwana wa Nebati, mtumwa wa Sulemani mwana wa Daudi, akainuka, akamfanyia fitina bwana wake. 7#Amu 9:4; Zab 26:4; Mit 12:11; Mdo 17:5Wakamkusanyikia watu mabaradhuli, wasiofaa kitu, waliojitia nguvu juu ya Rehoboamu mwana wa Sulemani, Rehoboamu alipokuwa kijana na wa moyo mwororo, asiweze kuwazuia. 8#Hos 8:6Hata sasa mwajidhania kuwa mtauzuia ufalme wa BWANA mikononi mwa wana wa Daudi; nanyi mmekuwa jamii kubwa, na kwenu mna ndama za dhahabu alizowafanyia Yeroboamu kuwa miungu. 9#2 Nya 11:14,15; Kut 29:35Je! Hamkuwafukuza makuhani wa BWANA, wana wa Haruni, na Walawi; mkajifanyia makuhani kama wafanyavyo watu wa nchi nyingine? Hata ye yote ajaye kujifanya wakfu na ndama, na kondoo waume saba, aweza kuwa kuhani wa hiyo isiyo miungu. 10Lakini sisi, BWANA ndiye Mungu wetu, wala sisi hatukumwacha; tena tunao makuhani wanaomtumikia BWANA, wana wa Haruni, na Walawi, kwa kazi yao; 11#2 Nya 2:4; Law 24:2-6; Kut 27:20,21nao humtolea BWANA kila asubuhi, na kila jioni, sadaka za kuteketezwa na fukizo la manukato; mikate ya wonyesho pia huiweka kwa taratibu yake juu ya meza takatifu, na kinara cha dhahabu chenye taa zake, kuwaka kila jioni; kwa maana sisi twayalinda malinzi ya BWANA, Mungu wetu; bali ninyi mmemwacha. 12#Kum 20:4; Yos 5:14; Zab 20:7; Hes 10:8; Ayu 15:25,26; Mdo 5:39; 9:4,5Na tazama, Mungu yu pamoja nasi atutangulie, na makuhani wake wenye mapanda, ili wapige sauti ya kugutusha juu yenu. Enyi wana wa Israeli, msipigane na BWANA, Mungu wa baba zenu; kwani hamtafanikiwa.
13Lakini Yeroboamu aliwazungushia waviziao kwa nyuma; basi wao wakawa mbele ya Yuda, na wale waviziao nyuma yao. 14Na Yuda walipotazama nyuma, angalia, vita vikawa mbele na nyuma; wakamlilia BWANA, na makuhani wakapiga mapanda. 15#Hes 32:4; 2 Nya 14:12Ndipo wakapiga kelele watu wa Yuda; ikawa, watu na Yuda walipopiga kelele, Mungu akampiga Yeroboamu na Israeli wote mbele ya Abiya na Yuda. 16Wana wa Israeli wakakimbia mbele ya Yuda; naye Mungu akawaua mikononi mwao. 17Abiya na watu wake wakawapiga mapigo makuu; hata wakaanguka wameuawa wa Israeli mia tano elfu, watu wateule. 18#Amu 8:28; 2 Fal 18:5; 1 Nya 5:20; 2 Nya 16:8,9; 20:20; Zab 22:5Ndivyo walivyotiishwa wana wa Israeli wakati ule, wakashinda wana wa Yuda, kwa kuwa walimtegemea BWANA, Mungu wa baba zao. 19#Yos 15:9; Yn 11:54Abiya akamfuata Yeroboamu, akamnyang’anya miji, Betheli na miji yake, na Yeshana na miji yake, na Efroni na miji yake. 20#1 Sam 25:38; 26:10; Eze 24:16; Mdo 12:23; 1 Fal 14:20Wala Yeroboamu hakupata nguvu tena siku za Abiya; kisha BWANA akampiga, akafa. 21Ila Abiya akapata nguvu, akaoa wake kumi na wanne, akazaa wana ishirini na wawili, na binti kumi na sita. 22#2 Nya 9:29; 12:15Na mambo ya Abiya yaliyosalia, na njia zake, na maneno yake, yameandikwa katika kitabu cha maelezo cha nabii Ido.

Iliyochaguliwa sasa

2 Nya 13: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia