Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Nya 12

12
Wamisri Waishambulia Yuda
1 # 2 Nya 11:17; Kum 8:14; 1 Fal 14:22-24 Ikawa ulipothibitika ufalme wa Rehoboamu, naye amepata nguvu, aliiacha torati ya BWANA, na Israeli wote pamoja naye. 2#1 Fal 14:24,25Ikawa katika mwaka wa tano wa mfalme Rehoboamu, akapanda Shishaki, mfalme wa Misri, juu ya Yerusalemu; kwa kuwa walikuwa wamemwasi BWANA; 3#2 Nya 16:8mwenye magari elfu moja na mia mbili, na wapanda farasi sitini elfu; na watu wasiohesabika, waliotoka Misri pamoja naye; Walubi, na Wasukii, na Wakushi. 4Akaitwaa miji yenye maboma iliyokuwa ya Yuda, akaja Yerusalemu. 5#2 Nya 11:2; Kum 28:25; 2 Nya 15:2Ndipo akaja Shemaya nabii kwa Rehoboamu, na kwa wakuu wa Yuda, waliokusanyika Yerusalemu kwa sababu ya Shishaki, akawaambia, BWANA asema hivi, Ninyi mmeniacha mimi, kwa hiyo nami nimewaacha ninyi mkononi mwa Shishaki. 6#Kut 10:3; Law 26:40-42; 2 Nya 33:12,19; 34:27; Zab 78:34; Yak 4:10; Kut 9:27Ndipo wakajinyenyekeza wakuu wa Israeli na mfalme; wakasema, BWANA ndiye mwenye haki. 7#1 Fal 21:28,29Naye BWANA alipoona ya kwamba wamejinyenyekeza, neno la BWANA likamjia Shemaya, kusema, Wamejinyenyekeza; sitawaharibu; lakini nitawapa wokovu punde, wala ghadhabu yangu haitamwagika juu ya Yerusalemu kwa mkono wa Shishaki. 8#Isa 26:13; Kum 28:47,48Walakini watamtumikia; ili wapate kujua utumwa wangu, na huo utumwa wa falme za nchi. 9#1 Fal 14:25,26; 10:16,17; 2 Nya 9:15,16Basi Shishaki, mfalme wa Misri, akapanda juu ya Yerusalemu, akazichukua hazina za nyumba ya BWANA, na hazina za nyumba ya mfalme; akazichukua zote. Akazichukua pia ngao za dhahabu alizozifanya Sulemani. 10#2 Sam 8:18; 23:23; 1 Nya 11:25Mfalme Rehoboamu akafanya ngao za shaba mahali pake, akawakabidhi wakuu wa walinzi, waliongoja mlangoni pa nyumba ya mfalme. 11Ikawa kila wakati mfalme alipoingia nyumbani mwa BWANA, wakaja walinzi wakazichukua, wakazirudisha tena chumbani mwa walinzi. 12#Mwa 18:24; 1 Fal 14:13; 2 Nya 19:3Naye alipojinyenyekeza, ghadhabu ya BWANA ikamgeukia mbali, asimharibu kabisa; tena yalionekana katika Yuda mambo mema. 13#1 Fal 14:21; 2 Nya 13:7; 2 Nya 6:6; Zab 48:1-3Basi mfalme Rehoboamu akajitia nguvu katika Yerusalemu, akatawala; maana Rehoboamu alikuwa na umri wa miaka arobaini na mmoja alipoanza kutawala, akatawala miaka kumi na saba huko Yerusalemu, mji aliouchagua BWANA miongoni mwa kabila zote za Israeli, ili aliweke huko jina lake. Na jina la mamaye aliitwa Naama Mwamoni. 14#Mt 7:7; Mdo 9:11Naye akatenda yaliyo maovu, kwa kuwa hakuukaza moyo wake amtafute BWANA. 15#2 Nya 9:29; 13:22Basi mambo yake Rehoboamu, ya kwanza na ya mwisho, je! Hayakuandikwa katika tarehe za Shemaya nabii na Ido mwonaji, kwa jinsi ya kuandika nasaba? Kulikuwa na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu siku zote. 16Rehoboamu akalala na babaze, akazikwa katika mji wa Daudi. Na Abiya mwanawe alitawala mahali pake.

Iliyochaguliwa sasa

2 Nya 12: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia