Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Kor 5

5
Uzinzi Hulichafua Kanisa
1 # Kum 22:30; Law 18:7,8 Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye. 2Nanyi mwajivuna, wala hamkusikitika, ili kwamba aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo. 3#Kol 2:5Kwa maana kweli, nisipokuwapo kwa mwili, lakini nikiwapo kwa roho, mimi mwenyewe nimekwisha kumhukumu yeye aliyetenda jambo hilo, kana kwamba nikiwapo. 4#Mt 16:19; 18:18; 2 Kor 13:10Katika jina la Bwana wetu Yesu, ninyi mkiwa mmekusanyika pamoja na roho yangu, pamoja na uweza wa Bwana wetu Yesu; 5#1 Tim 1:20; 1 Pet 4:6kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu. 6#Gal 5:9Kujisifu kwenu si kuzuri. Hamjui kwamba chachu kidogo hulichachusha donge zima? 7#Kut 12:5,21; 13:7; Isa 53:7; 1 Pet 1:19Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo; 8#Kut 13:7; 12:3-20; Kum 16:3basi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochachika, ndio weupe wa moyo na kweli.
Uzinzi hauna budi Kuhukumiwa
9 # Mt 18:17; 2 The 3:14 Naliwaandikia katika waraka wangu, kwamba msichangamane na wazinzi. 10Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang’anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia. 11#2 The 3:6; Tit 3:10; 2 Yoh 1:10Lakini, mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang’anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye. 12#Mk 4:11Maana yanihusu nini kuwahukumu wale walio nje? Ninyi hamwahukumu hao walio ndani? 13#Kum 13:5; 17:7; 22:24Lakini hao walio nje Mungu atawahukumu. Ninyi mwondoeni yule mbaya miongoni mwenu. u.

Iliyochaguliwa sasa

1 Kor 5: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha