Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Kor 4

4
Huduma ya Mitume
1 # Tit 1:7 Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu. 2#Lk 12:42Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu. 3Lakini, kwangu mimi, si kitu kabisa nihukumiwe na ninyi, wala kwa hukumu ya kibinadamu, wala sijihukumu hata nafsi yangu. 4#Zab 143:2Maana sijui sababu ya kujishitaki nafsi yangu, lakini sihesabiwi haki kwa ajili hiyo; ila anihukumuye mimi ni Bwana. 5#1 Kor 3:8Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulikisha yaliyositirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.
6 # Rum 12:3 Basi ndugu, mambo hayo nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na Apolo kwa ajili yenu, ili kwamba kwa mfano wetu mpate kujifunza kutokupita yale yaliyoandikwa; ili mmoja wenu asijivune kwa ajili ya huyu, kinyume cha mwenziwe. 7#Rum 12:6Maana ni nani anayekupambanua na mwingine? Nawe una nini usichokipokea? Lakini iwapo ulipokea, wajisifia nini kana kwamba hukupokea? 8#Ufu 3:17,21Mmekwisha kushiba, mmekwisha kupata utajiri, mmemiliki pasipo sisi. Naam, laiti mngemiliki, ili sisi nasi tumiliki pamoja nanyi! 9#Rum 8:36; Ebr 10:33Maana nadhani ya kuwa Mungu ametutoa sisi mitume mwisho, kama watu waliohukumiwa wauawe; kwa sababu tumekuwa tamasha kwa dunia; kwa malaika na wanadamu. 10#1 Kor 3:18Sisi tu wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi ni wenye akili katika Kristo; sisi tu dhaifu, lakini ninyi mna nguvu; ninyi mna utukufu, lakini sisi hatupati heshima. 11#2 Kor 11:23-27Hata saa hii ya sasa, tuna njaa na kiu, tu uchi, twapigwa ngumi, tena hatuna makao; 12#Mdo 18:3; 20:34; 1 The 2:9; 2 The 3:8; Rum 12:14; 1 Kor 9:15; Zab 109:28kisha twataabika tukifanya kazi kwa mikono yetu wenyewe. Tukitukanwa twabariki, tukiudhiwa twastahimili; 13#Kum 17:7; 22:24tukisingiziwa twasihi; tumefanywa kama takataka za dunia, na tama ya vitu vyote hata sasa.
14Siyaandiki hayo ili kuwatahayarisha; bali kuwaonya kama watoto niwapendao. 15#Gal 4:19Kwa kuwa ijapokuwa mna waalimu kumi elfu katika Kristo, walakini hamna baba wengi. Maana mimi ndimi niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili. 16#1 Kor 11:1; Flp 3:17Basi, nawasihi mnifuate mimi. 17#Mdo 19:22; Flp 2:20Kwa sababu hii nimemtuma Timotheo kwenu, aliye mwanangu mpendwa, mwaminifu katika Bwana, atakayewakumbusha njia zangu zilizo katika Kristo, kama vile nifundishavyo kila mahali katika kila kanisa. 18Basi wengine wamejivuna kana kwamba siji kwenu. 19#Mdo 18:21; Yak 4:15Lakini nitakuja kwenu upesi, nikijaliwa, nami nitafahamu, si neno lao tu waliojivuna, bali nguvu zao. 20#1 Kor 2:4; Lk 17:20Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu. 21Mnataka vipi? Nije kwenu na fimbo, au nije katika upendo na roho ya upole?

Iliyochaguliwa sasa

1 Kor 4: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia