Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Kor 14:34-40

1 Kor 14:34-40 SUV

Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo. Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa. Au je! Neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu? Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue hayo ninayowaandikia, ya kwamba ni maagizo ya Bwana. Lakini mtu akiwa mjinga, na awe mjinga. Kwa ajili ya hayo, ndugu, takeni sana kuhutubu, wala msizuie kunena kwa lugha. Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu.