1 Wakorintho 14:34-40
1 Wakorintho 14:34-40 NENO
wanawake wanapaswa kuwa kimya katika kundi la waumini. Hawaruhusiwi kusema, bali wanyenyekee kama Torati isemavyo. Wakitaka kuuliza kuhusu jambo lolote, wawaulize waume zao nyumbani. Kwa maana ni aibu kwa mwanamke kuzungumza katika kundi la waumini. Je, neno la Mungu lilianzia kwenu? Au ni ninyi tu ambao neno la Mungu limewafikia? Kama mtu yeyote akidhani kwamba yeye ni nabii, au ana karama za rohoni, basi na akubali kwamba haya ninayoandika ni maagizo kutoka kwa Bwana Isa. Kama mtu akipuuza jambo hili yeye mwenyewe atapuuzwa. Kwa hiyo ndugu zangu, takeni sana kutoa unabii na msikataze watu kusema kwa lugha. Lakini kila kitu kitendeke kwa ufasaha na kwa utaratibu.