Zekaria 8:1-8
Zekaria 8:1-8 NENO
Neno la BWANA wa majeshi likanijia tena. Hili ndilo asemalo BWANA wa majeshi: “Nina wivu sana kwa ajili ya Sayuni, ninawaka wivu kwa ajili yake.” Hili ndilo asemalo BWANA: “Nitarudi Sayuni na kufanya makao Yerusalemu. Kisha Yerusalemu utaitwa mji wa kweli, mlima wa BWANA wa majeshi utaitwa Mlima Mtakatifu.” Hili ndilo asemalo BWANA wa majeshi: “Kwa mara nyingine tena wanaume na wanawake walioshiba umri wataketi katika barabara za Yerusalemu, kila mmoja akiwa na mkongojo wake mkononi kwa sababu ya umri wake. Barabara za mji zitajaa wavulana na wasichana wanaocheza humo.” Hili ndilo asemalo BWANA wa majeshi: “Mambo haya yanaweza kuonekana ya ajabu kwa mabaki ya watu wakati huo, lakini yaweza kuwa ya ajabu kwangu?” asema BWANA wa majeshi. Hili ndilo asemalo BWANA wa majeshi: “Nitawaokoa watu wangu kutoka nchi za mashariki na magharibi. Nitawarudisha waje kuishi Yerusalemu, watakuwa watu wangu nami nitakuwa mwaminifu na wa haki kwao kama Mungu wao.”