Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ufunuo 18:18-24

Ufunuo 18:18-24 NEN

Watakapouona moshi wa kuungua kwake watalia wakisema, ‘Je, kulipata kuwako mji mkubwa kama huu?’ Nao watajirushia mavumbi vichwani mwao, huku wakilia na kuomboleza, wakisema: “ ‘Ole! Ole, ee mji mkubwa, mji ambao wote wenye meli baharini walitajirika kupitia kwa mali zake! Katika saa moja tu ameangamizwa! Furahia kwa ajili yake, ee mbingu! Furahini watakatifu, mitume na manabii! Mungu amemhukumu kwa vile alivyowatendea ninyi.’ ” Kisha malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe kubwa kama la kusagia akalitupa baharini akisema: “Hivyo ndivyo mji mkubwa Babeli utakavyotupwa chini kwa nguvu wala hautaonekana tena. Nyimbo za wapiga vinubi na waimbaji, wapiga filimbi na wapiga tarumbeta kamwe hazitasikika tena ndani yako. Ndani yako kamwe hataonekana tena fundi mwenye ujuzi wa aina yoyote. Wala sauti ya jiwe la kusagia kamwe haitasikika tena. Mwanga wa taa hautaangaza ndani yako tena. Sauti ya bwana arusi na bibi arusi kamwe haitasikika ndani yako tena. Wafanyabiashara wako walikuwa watu maarufu wa dunia. Mataifa yote yalipotoshwa kwa uchawi wako. Ndani yake ilionekana damu ya manabii na ya watakatifu na wote waliouawa duniani.”

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Ufunuo 18:18-24

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha