Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 95:1-6

Zaburi 95:1-6 NEN

Njooni, tumwimbie BWANA kwa furaha; tumfanyie kelele za shangwe Mwamba wa wokovu wetu. Tuje mbele zake kwa shukrani, tumtukuze kwa vinanda na nyimbo. Kwa kuwa BWANA ni Mungu mkuu, mfalme mkuu juu ya miungu yote. Mkononi mwake mna vilindi vya dunia, na vilele vya milima ni mali yake. Bahari ni yake, kwani ndiye aliifanya, na mikono yake iliumba nchi kavu. Njooni, tusujudu, tumwabudu, tupige magoti mbele za BWANA Muumba wetu

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 95:1-6