Zaburi 95:1-6
Zaburi 95:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Njoni tumwimbie Mwenyezi-Mungu, tumshangilie mwamba wa wokovu wetu! Twende mbele zake na shukrani; tumshangilie kwa nyimbo za sifa. Maana Mwenyezi-Mungu, ni Mungu mkuu; yeye ni Mfalme mkuu juu ya miungu yote. Vilindi vyote vya dunia vimo mikononi mwake, vilele vya milima ni vyake. Bahari ni yake, ndiye aliyeifanya; kwa mikono yake aliiumba nchi kavu. Njoni tusujudu na kumwabudu; tumpigie magoti Mwenyezi-Mungu, Muumba wetu!
Zaburi 95:1-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Njoni, tumwimbie BWANA, Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu. Tuje mbele zake kwa shukrani, Tumfanyie shangwe kwa zaburi. Kwa kuwa BWANA ni Mungu mkuu, Na Mfalme mkuu juu ya miungu yote. Mkononi mwake zimo bonde za dunia, Hata vilele vya milima ni vyake. Bahari ni yake, ndiye aliyeifanya, Na mikono yake iliumba nchi kavu. Njoni, tuabudu, tusujudu, Tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba.
Zaburi 95:1-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Njoni, tumwimbie BWANA, Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu. Tuje mbele zake kwa shukrani, Tumfanyie shangwe kwa zaburi. Kwa kuwa BWANA ni Mungu mkuu, Na Mfalme mkuu juu ya miungu yote. Mkononi mwake zimo bonde za dunia, Hata vilele vya milima ni vyake. Bahari ni yake, ndiye aliyeifanya, Na mikono yake iliumba nchi kavu. Njoni, tuabudu, tusujudu, Tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba.
Zaburi 95:1-6 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Njooni, tumwimbie BWANA kwa furaha; tumfanyie kelele za shangwe Mwamba wa wokovu wetu. Tuje mbele zake kwa shukrani, tumtukuze kwa vinanda na nyimbo. Kwa kuwa BWANA ni Mungu mkuu, mfalme mkuu juu ya miungu yote. Mkononi mwake mna vilindi vya dunia, na vilele vya milima ni mali yake. Bahari ni yake, kwani ndiye aliifanya, na mikono yake iliumba nchi kavu. Njooni, tusujudu, tumwabudu, tupige magoti mbele za BWANA Muumba wetu