Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 9:11-20

Zaburi 9:11-20 NENO

Mwimbieni Mwenyezi Mungu sifa, amefanywa mtawala Sayuni, tangazeni miongoni mwa mataifa, yale aliyoyatenda. Kwa maana yeye anayelipiza kisasi cha damu hukumbuka, hapuuzi kilio cha wanaoonewa. Ee Mwenyezi Mungu, tazama jinsi walivyo wengi adui zangu wanaonitesa! Nihurumie, uniinue kutoka malango ya mauti, ili niweze kutangaza sifa zako katika malango ya Binti Sayuni, na huko niushangilie wokovu wako. Mataifa wameanguka kwenye shimo walilolichimba, miguu yao imenaswa kwenye wavu waliouficha. Mwenyezi Mungu anajulikana kwa haki yake, waovu wamenaswa katika kazi za mikono yao. Waovu wataishia Kuzimu, naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu. Lakini mhitaji hatasahaulika siku zote, wala matumaini ya walioonewa hayatapotea. Ee Mwenyezi Mungu, inuka, usimwache binadamu ashinde. Mataifa na yahukumiwe mbele zako. Ee Mwenyezi Mungu, wapige kwa hofu, mataifa na yajue kuwa wao ni watu tu.