Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 81

81
Zaburi 81
Wimbo wa sikukuu
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya Asafu.
1Mwimbieni kwa furaha, Mungu aliye nguvu yetu;
mpigieni kelele za shangwe Mungu wa Yakobo!
2Anzeni wimbo, pigeni matari,
pigeni kinubi na zeze kwa sauti nzuri.
3Pigeni baragumu za pembe za kondoo dume
wakati wa Mwandamo wa Mwezi,
na wakati wa mwezi mpevu,
katika siku ya Sikukuu yetu;
4hii ni amri kwa Israeli,
agizo la Mungu wa Yakobo.
5Aliiweka iwe kama sheria kwa Yusufu
alipotoka dhidi ya Misri,
huko tulikosikia lugha ambayo hatukuielewa.
6Asema, “Nimeondoa mzigo mabegani mwao;
mikono yao iliwekwa huru kutoka kwa kikapu.
7Katika shida yako uliniita nami nikakuokoa,
nilikujibu katika mawingu yenye ngurumo;
nilikujaribu katika maji ya Meriba.
8“Enyi watu wangu, sikieni, nami nitawaonya:
laiti kama mngenisikiliza, ee Israeli!
9Hamtakuwa na mungu mgeni miongoni mwenu;
msimsujudie mungu wa kigeni.
10Mimi ni Mwenyezi Mungu, Mungu wako,
niliyekutoa nchi ya Misri.
Panua sana kinywa chako
nami nitakijaza.
11“Lakini watu wangu hawakunisikiliza;
Israeli hakunitii.
12Basi niliwaacha katika ukaidi wa mioyo yao
wafuate mashauri yao wenyewe.
13“Laiti watu wangu wangenisikiliza,
laiti Israeli wangefuata njia zangu,
14ningewatiisha adui zao kwa haraka,
na kuugeuza mkono wangu dhidi ya watesi wao!
15Wale wanaomchukia Mwenyezi Mungu wangejikunyata mbele zake,
na adhabu yao ingedumu milele.
16Bali ninyi mngelishwa ngano iliyo bora,
na kuwatosheleza kwa asali inayotoka kwenye mwamba.”

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 81: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia