Zaburi 78:9-16
Zaburi 78:9-16 NENO
Watu wa Efraimu, ingawa walijifunga pinde, walikimbia siku ya vita. Hawakulishika agano la Mungu, na walikataa kuishi kwa sheria yake. Walisahau aliyokuwa ameyatenda, maajabu aliyokuwa amewaonesha. Alitenda miujiza machoni mwa baba zao, huko Soani, katika nchi ya Misri. Aliigawanya bahari akawapitisha, alifanya maji yasimame imara kama ukuta. Aliwaongoza kwa wingu mchana, na kwa nuru ya moto usiku kucha. Alipasua miamba jangwani na akawapa maji tele kama bahari, alitoa vijito kutoka jabali lililochongoka, akayafanya maji yatiririke kama mito.