Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 73:21-26

Zaburi 73:21-26 NEN

Wakati moyo wangu ulipohuzunishwa, na roho yangu ilipotiwa uchungu, nilikuwa mpumbavu na mjinga, nilikuwa mnyama mkatili mbele yako. Hata hivyo niko pamoja nawe siku zote, umenishika mkono wangu wa kuume. Unaniongoza kwa shauri lako, hatimaye utaniingiza katika utukufu. Nani niliye naye mbinguni ila wewe? Dunia haina chochote ninachokitamani ila wewe. Mwili na moyo wangu vyaweza kushindwa, bali Mungu ni nguvu ya moyo wangu na fungu langu milele.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 73:21-26