Zaburi 46:1-7
Zaburi 46:1-7 NEN
Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa, hata kama dunia ikiondolewa nayo milima ikiangukia moyoni mwa bahari. Hata kama maji yake yatanguruma na kuumuka, milima nayo ikitetemeka kwa mawimbi yake. Kuna mto ambao vijito vyake vinaufurahisha mji wa Mungu, mahali patakatifu ambako Aliye Juu Sana anaishi. Mungu yuko katikati yake, hautaanguka, Mungu atausaidia asubuhi na mapema. Mataifa yanafanya ghasia, falme zinaanguka, Yeye huinua sauti yake, dunia ikayeyuka. BWANA Mwenye Nguvu Zote yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.