Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 24:1-6

Zaburi 24:1-6 NEN

Dunia ni mali ya BWANA, na vyote vilivyomo ndani yake, ulimwengu, na wote waishio ndani yake, maana aliiwekea misingi yake baharini na kuifanya imara juu ya maji. Nani awezaye kuupanda mlima wa BWANA? Ni nani awezaye kusimama patakatifu pake? Ni yule mwenye mikono safi na moyo mweupe, yule ambaye hakuinulia sanamu nafsi yake au kuapa kwa kitu cha uongo. Huyo atapokea baraka kutoka kwa BWANA, na hukumu ya haki kutoka kwa Mungu Mwokozi wake. Hiki ndicho kizazi cha wale wamtafutao, wale wautafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.