Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 24:1-6

Zaburi 24:1-6 BHN

Dunia na vyote vilivyomo ni vyake Mwenyezi-Mungu; ulimwengu na wote waishio humo ni mali yake. Maana yeye aliweka misingi ya dunia juu ya bahari; aliisimika imara juu ya mito ya maji. Nani atakayepanda mlima wa Mwenyezi-Mungu? Nani atakayekaa katika hekalu lake takatifu? Ni mtu wa matendo mema na moyo safi, asiyeuelekeza moyo wake katika upuuzi, wala kuapa kwa uongo. Mtu huyo atapokea baraka kwa Mwenyezi-Mungu, na haki yake kwa Mungu mwokozi wake. Ndio hali ya kizazi cha watu wamtafutao yeye; naam, watu wamtafutao Mungu wa Yakobo.

Soma Zaburi 24