Zaburi 19:7-14
Zaburi 19:7-14 NENO
Torati ya Mwenyezi Mungu ni kamilifu, ikihuisha nafsi. Shuhuda za Mwenyezi Mungu ni za kuaminika, zikimpa mjinga hekima. Maagizo ya Mwenyezi Mungu ni kamili, nayo hufurahisha moyo. Amri za Mwenyezi Mungu huangaza, zatia nuru machoni. Kumcha Mwenyezi Mungu ni utakatifu, nako kwadumu milele. Amri za Mwenyezi Mungu ni za hakika, nazo zina haki. Ni za thamani kuliko dhahabu, kuliko dhahabu iliyo safi sana, ni tamu kuliko asali, kuliko asali kutoka sega. Kwa hizo mtumishi wako anaonywa, katika kuzishika kuna thawabu kubwa. Ni nani awezaye kutambua makosa yake? Nisamehe makosa yangu nisiyoyajua. Mlinde mtumishi wako na dhambi za makusudi, nazo zisinitawale. Ndipo nitakapokuwa sina lawama, niwe huru na hatia kubwa. Maneno ya kinywa changu na mawazo ya moyo wangu, yapate kibali mbele zako, Ee Mwenyezi Mungu, Mwamba wangu na Mkombozi wangu.