Zaburi 118:20-24
Zaburi 118:20-24 NENO
Hili ni lango la Mwenyezi Mungu ambalo wenye haki wanaweza kuliingia. Nitakushukuru, kwa kuwa ulinijibu, umekuwa wokovu wangu. Jiwe walilolikataa waashi, limekuwa jiwe kuu la pembeni. Mwenyezi Mungu ametenda hili, nalo ni la kushangaza machoni petu. Hii ndiyo siku Mwenyezi Mungu aliyoifanya, tushangilie na kufurahi ndani yake.