Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 10:14-18

Zaburi 10:14-18 NEN

Lakini wewe, Ee Mungu, unaona shida na huzuni, umekubali kuyapokea mkononi mwako. Mhanga anajisalimisha kwako, wewe ni msaada wa yatima. Vunja mkono wa mtu mwovu na mbaya, mwite atoe hesabu ya maovu yake ambayo yasingejulikana. BWANA ni Mfalme milele na milele, mataifa wataangamia watoke nchini mwake. Unasikia, Ee BWANA, shauku ya wanaoonewa, wewe huwatia moyo, na kusikiliza kilio chao, ukiwatetea yatima na walioonewa, ili mwanadamu, ambaye ni udongo, asiogopeshe tena.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 10:14-18