Zaburi 10:14-18
Zaburi 10:14-18 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini wewe wawaona wenye dhiki na shida; nawe daima uko tayari kuwasaidia. Mnyonge anakutegemea wewe, ee Mungu, wewe umekuwa daima msaada wa yatima. Uzivunje nguvu za mtu mwovu; ukomeshe uovu wake wote, usiwepo tena. Mwenyezi-Mungu ni mfalme milele na milele! Mataifa yasiyomjua yatatoweka nchini mwake. Ee Mwenyezi-Mungu, wapokea dua za mnyonge; wampa moyo na kumtegea sikio. Utawatendea haki yatima na wanaodhulumiwa, binadamu aliye udongo asiweze tena kuleta hofu.
Zaburi 10:14-18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Umeona, maana unaangalia matatizo na dhiki, Uyatwae mkononi mwako. Mtu duni hukuachia nafsi yake, Maana umekuwa msaidizi wa yatima. Uuvunje mkono wa mdhalimu, Na mwovu, uipatilize dhuluma yake, hadi usiione. BWANA ndiye Mfalme milele na milele; Mataifa yataangamia kutoka nchi yake. BWANA, utayasikia matakwa ya wanyonge, Uutaidhibiti mioyo yao, utalitega sikio lako. Ili kumhukumu yatima na aliyeonewa, Binadamu aliye udongo asizidi kudhulumu.
Zaburi 10:14-18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Umeona, maana unaangalia madhara na jeuri, Uyatwae mkononi mwako. Mtu duni hukuachia nafsi yake, Maana umekuwa msaidizi wa yatima. Uuvunje mkono wake mdhalimu, Na mbaya, uipatilize dhuluma yake, hata usiione. BWANA ndiye Mfalme milele na milele; Mataifa wamepotea kutoka nchi yake. BWANA, umeisikia tamaa ya wanyonge, Utaitengeneza mioyo yao, utalitega sikio lako. Ili kumhukumu yatima naye aliyeonewa, Binadamu aliye udongo asizidi kudhulumu.
Zaburi 10:14-18 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Lakini wewe, Ee Mungu, unaona shida na huzuni, umekubali kuyapokea mkononi mwako. Mhanga anajisalimisha kwako, wewe ni msaada wa yatima. Vunja mkono wa mtu mwovu na mbaya, mwite atoe hesabu ya maovu yake ambayo yasingejulikana. BWANA ni Mfalme milele na milele, mataifa wataangamia watoke nchini mwake. Unasikia, Ee BWANA, shauku ya wanaoonewa, wewe huwatia moyo, na kusikiliza kilio chao, ukiwatetea yatima na walioonewa, ili mwanadamu, ambaye ni udongo, asiogopeshe tena.