Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 30:24-33

Mithali 30:24-33 NEN

“Vitu vinne duniani vilivyo vidogo, lakini vina akili nyingi sana: Mchwa ni viumbe wenye nguvu ndogo, hata hivyo hujiwekea akiba ya chakula chao wakati wa kiangazi. Pelele ni viumbe vyenye uwezo mdogo hata hivyo hujitengenezea nyumba zao kwenye miamba. Nzige hawana mfalme, hata hivyo huenda pamoja vikosi vikosi. Mjusi anaweza kushikwa kwa mkono, hata hivyo huonekana katika majumba ya kifalme. “Viko vitu vitatu ambavyo vinapendeza katika mwendo wao, naam, vinne ambavyo hutembea kwa mwendo wa madaha: simba, mwenye nguvu miongoni mwa wanyama, asiyerudi nyuma kwa chochote; jogoo atembeaye kwa maringo, pia beberu, naye mfalme pamoja na jeshi lake lililomzunguka. “Ikiwa umefanya upumbavu na ukajitukuza mwenyewe, au kama umepanga mabaya, basi funika mdomo wako na mkono wako. Kwa maana kama vile kusukasuka maziwa hutoa siagi, na pia kule kufinya pua hutoa damu, kadhalika kuchochea hasira hutokeza ugomvi.”