Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 19:1-12

Mithali 19:1-12 NENO

Afadhali mtu maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama, kuliko mpumbavu ambaye midomo yake imepotoka. Sio vizuri kuwa na juhudi bila maarifa, wala kufanya haraka na kuikosa njia. Upumbavu wa mtu mwenyewe huharibu maisha yake hata hivyo moyo wake humkasirikia Mwenyezi Mungu. Mali huleta rafiki wengi, bali rafiki wa mtu maskini humwacha. Shahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa, naye amwagaye uongo hataachwa huru. Wengi hujipendekeza kwa mtawala na kila mmoja ni rafiki wa mtu atoaye zawadi. Mtu maskini huepukwa na ndugu zake wote: Je, rafiki zake watamkwepa kiasi gani! Ingawa huwafuata kwa kuwasihi, hawapatikani popote. Yeye apataye hekima huipenda nafsi yake mwenyewe, yeye ahifadhiye ufahamu hustawi. Shahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa, naye amwagaye uongo ataangamia. Haistahili mpumbavu kuishi katika anasa, itakuwa vibaya kiasi gani kwa mtumwa kuwatawala wakuu. Hekima ya mtu humpa uvumilivu, ni kwa utukufu wake kusamehe makosa. Ghadhabu ya mfalme ni kama mngurumo wa simba, bali wema wake ni kama umande juu ya nyasi.