Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 15:1-9

Mithali 15:1-9 NEN

Jawabu la upole hugeuza ghadhabu, bali neno liumizalo huchochea hasira. Ulimi wa mwenye hekima husifu maarifa, bali kinywa cha mpumbavu hufoka upumbavu. Macho ya BWANA yako kila mahali, yakiwaangalia waovu na wema. Ulimi uletao uponyaji ni mti wa uzima, bali ulimi udanganyao huponda roho. Mpumbavu hubeza maonyo ya baba yake, bali yeyote akubaliye maonyo huonyesha busara. Nyumba ya mwenye haki ina hazina kubwa, bali mapato ya waovu huwaletea taabu. Midomo ya mwenye hekima hueneza maarifa, bali sivyo ilivyo mioyo ya wapumbavu. BWANA huchukia sana dhabihu za waovu, bali maombi ya wanyofu humfurahisha Mungu. BWANA huchukia sana njia ya waovu, bali huwapenda wale wafuatao haki.