Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 14:29-33

Mithali 14:29-33 NENO

Mtu mwenye subira ana ufahamu mwingi, bali anayekasirika haraka huonesha upumbavu. Moyo wenye amani huupa mwili uzima, bali wivu huozesha mifupa. Yeye anayemdhulumu maskini humdharau Muumba wao, bali yeyote anayemhurumia mhitaji humheshimu Mungu. Waovu huangamizwa kwa matendo yao maovu, bali hata katika kifo wenye haki hupata kimbilio. Hekima hukaa katika moyo wa mwenye ufahamu bali haijulikani miongoni mwa wapumbavu.