Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 1:10-16

Mithali 1:10-16 NENO

Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, usikubaliane nao. Wakisema, “Twende tufuatane; tukamvizie mtu na kumwaga damu, njoo tukavizie nafsi isiyo na hatia; tuwameze wakiwa hai kama kaburi, wakiwa wazima kama wale wanaotumbukia shimoni. Tutapata aina zote za vitu vya thamani na kujaza nyumba zetu kwa nyara. Njoo ushirikiane nasi, vitu vyote tutakavyopata tutagawana.” Mwanangu, usiandamane nao. Usiweke mguu wako katika njia zao, kwa kuwa miguu yao hukimbilia kwenye dhambi, ni wepesi kumwaga damu.