Hesabu 7
7
Sadaka za kuweka wakfu Maskani ya Mwenyezi Mungu
1Musa alipomaliza kuisimamisha Maskani, aliipaka mafuta na kuiweka wakfu pamoja na samani zake zote. Pia alitia madhabahu mafuta na kuiweka wakfu, pamoja na vyombo vyake vyote. 2Ndipo viongozi wa Israeli, wale wakuu wa jamaa waliokuwa viongozi wa kabila wasimamizi wa wale waliohesabiwa, wakatoa sadaka. 3Walizileta kama matoleo yao mbele za Mwenyezi Mungu: magari sita ya kukokotwa yaliyofunikwa, pamoja na maksai kumi na wawili; yaani maksai mmoja kutoka kwa kila kiongozi, na gari moja la kukokotwa kutoka kwa kila viongozi wawili. Haya waliyaleta mbele ya Maskani.
4Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, 5“Vikubali vitu hivi kutoka kwao, ili viweze kutumika katika kazi kwenye Hema la Kukutania. Wapatie Walawi kama kazi ya kila mtu itakavyohitaji.”
6Hivyo Musa akachukua yale magari ya kukokotwa pamoja na maksai, na kuwapa Walawi. 7Aliwapa Wagershoni magari mawili ya kukokotwa na maksai wanne, kama walivyohitaji kwa kazi yao, 8na pia aliwapa Wamerari magari manne ya kukokotwa na maksai wanane, kama kazi yao ilivyohitaji. Wote walikuwa chini ya maelekezo ya Ithamari mwana wa kuhani, Haruni. 9Lakini Musa hakuwapa Wakohathi chochote kati ya hivyo, kwa sababu walitakiwa kubeba vitu vitakatifu mabegani mwao, vile walikuwa wanawajibika.
10Madhabahu yalipopakwa mafuta, viongozi walileta sadaka zao kwa ajili ya kule kuwekwa wakfu kwake na kuziweka mbele ya madhabahu. 11Kwa maana Mwenyezi Mungu alikuwa amemwambia Musa, “Kila siku kiongozi mmoja ataleta sadaka yake ili kuwekwa wakfu madhabahu.”
12Yule ambaye alileta sadaka yake siku ya kwanza alikuwa Nashoni, mwana wa Aminadabu, wa kabila la Yuda.
13Sadaka yake ilikuwa:
sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli mia moja na thelathini#7:13 Shekeli 130 za fedha ni sawa na kilo 1.5., na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini#7:13 Shekeli 70 za fedha ni sawa gramu 800., vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya nafaka;
14sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi#7:14 Shekeli 10 za dhahabu ni sawa na gramu 110., likiwa limejazwa uvumba;
15fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;
16beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;
17maksai wawili, kondoo dume watano, beberu watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani.
Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Nashoni mwana wa Aminadabu.
18Siku ya pili yake Nethaneli mwana wa Suari, kiongozi wa Isakari, alileta sadaka yake.
19Sadaka aliyoleta ilikuwa:
sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya nafaka;
20sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;
21fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;
22beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;
23maksai wawili, kondoo dume watano, beberu watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani.
Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Nethaneli mwana wa Suari.
24Siku ya tatu Eliabu mwana wa Heloni, kiongozi wa watu wa Zabuloni, alileta sadaka yake.
25Sadaka aliyoleta ilikuwa:
sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya nafaka;
26sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;
27fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;
28beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;
29maksai wawili, kondoo dume watano, beberu watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani.
Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Eliabu mwana wa Heloni.
30Siku ya nne Elisuri mwana wa Shedeuri, kiongozi wa watu wa Reubeni, alileta sadaka yake.
31Sadaka aliyoleta ilikuwa:
sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya nafaka;
32sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;
33fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;
34beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;
35maksai wawili, kondoo dume watano, beberu watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani.
Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Elisuri mwana wa Shedeuri.
36Siku ya tano Shelumieli mwana wa Surishadai, kiongozi wa watu wa Simeoni, alileta sadaka yake.
37Sadaka aliyoleta ilikuwa:
sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya nafaka;
38sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;
39fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;
40beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;
41maksai wawili, kondoo dume watano, beberu watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani.
Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Shelumieli mwana wa Surishadai.
42Siku ya sita Eliasafu mwana wa Deueli, kiongozi wa watu wa Gadi, alileta sadaka yake.
43Sadaka aliyoleta ilikuwa:
sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya nafaka;
44sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;
45fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;
46beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;
47maksai wawili, kondoo dume watano, beberu watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani.
Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Eliasafu mwana wa Deueli.
48Siku ya saba Elishama mwana wa Amihudi, kiongozi wa watu wa Efraimu, alileta sadaka yake.
49Sadaka aliyoleta ilikuwa:
sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya nafaka;
50sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;
51fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;
52beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;
53maksai wawili, kondoo dume watano, beberu watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani.
Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Elishama mwana wa Amihudi.
54Siku ya nane Gamalieli mwana wa Pedasuri, kiongozi wa watu wa Manase, alileta sadaka yake.
55Sadaka aliyoleta ilikuwa:
sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya nafaka;
56sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;
57fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;
58beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;
59maksai wawili, kondoo dume watano, beberu watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani.
Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Gamalieli mwana wa Pedasuri.
60Siku ya tisa Abidani mwana wa Gideoni, kiongozi wa watu wa Benyamini, alileta sadaka yake.
61Sadaka aliyoleta ilikuwa:
sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya nafaka;
62sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;
63fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;
64beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;
65maksai wawili, kondoo dume watano, beberu watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani.
Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Abidani mwana wa Gideoni.
66Siku ya kumi Ahiezeri mwana wa Amishadai, kiongozi wa watu wa Dani, alileta sadaka yake.
67Sadaka aliyoleta ilikuwa:
sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya nafaka;
68sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;
69fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;
70beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;
71maksai wawili, kondoo dume watano, beberu watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani.
Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Ahiezeri mwana wa Amishadai.
72Siku ya kumi na moja Pagieli mwana wa Okrani, kiongozi wa watu wa Asheri, alileta sadaka yake.
73Sadaka aliyoleta ilikuwa:
sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya nafaka;
74sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;
75fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;
76beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;
77maksai wawili, kondoo dume watano, beberu watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani.
Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Pagieli mwana wa Okrani.
78Siku ya kumi na mbili Ahira mwana wa Enani, kiongozi wa watu wa Naftali, alileta sadaka yake.
79Sadaka aliyoleta ilikuwa:
sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya nafaka;
80sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;
81fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;
82beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;
83maksai wawili, kondoo dume watano, beberu watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani.
Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Ahira mwana wa Enani.
84Hizi ndizo sadaka zilizotolewa na viongozi wa Israeli madhabahu yalipowekwa wakfu, wakati yalipakwa mafuta:
sahani kumi na mbili za fedha, bakuli kumi na mbili za fedha za kunyunyizia, na masinia kumi na mawili ya dhahabu. 85Kila sahani ya fedha ilikuwa na uzito wa shekeli mia moja na thelathini, na kila bakuli la fedha la kunyunyizia lilikuwa na uzito wa shekeli sabini. Masinia yote kumi na mawili yalikuwa na uzito wa shekeli elfu mbili na mia nne#7:85 Shekeli 2,400 za fedha ni sawa na kilo 28. kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. 86Sahani kumi na mbili za dhahabu zilizojazwa uvumba zilikuwa na uzito wa shekeli kumi kila moja, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. Kwa jumla, sahani za dhahabu zilikuwa na uzito wa shekeli mia moja na ishirini#7:86 Shekeli 120 za dhahabu ni sawa na kilo 1.4..
87Jumla ya wanyama waliotolewa kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa walikuwa fahali kumi na wawili wachanga, kondoo dume kumi na wawili, na wana-kondoo dume kumi na wawili wa mwaka mmoja, pamoja na sadaka zao za nafaka. Beberu kumi na wawili walitolewa kwa ajili ya sadaka za dhambi.
88Jumla ya wanyama kwa ajili ya dhabihu ya sadaka ya amani walikuwa maksai ishirini na wanne, kondoo dume sitini, beberu wa mwaka mmoja sitini, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja sitini.
Hizo ndizo sadaka zilizoletwa kwa ajili ya kuwekwa wakfu kwa madhabahu baada ya kupakwa mafuta.
89Musa alipoingia kwenye Hema la Kukutania kuzungumza na Mwenyezi Mungu, alisikia sauti ikisema naye kutoka kati ya wale makerubi wawili waliokuwa juu ya kile kiti cha rehema, juu ya Sanduku la Ushuhuda. Musa akazungumza na Mwenyezi Mungu.
Iliyochaguliwa sasa
Hesabu 7: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.