Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mathayo 8:1-4

Mathayo 8:1-4 NEN

Yesu aliposhuka kutoka mlimani, makutano makubwa ya watu yakamfuata. Mtu mmoja mwenye ukoma akaja na kupiga magoti mbele yake, akasema, “Bwana, kama ukitaka, unaweza kunitakasa.” Yesu akanyoosha mkono wake akamgusa yule mtu, akamwambia, “Nataka. Takasika!” Mara yule mtu akatakasika ukoma wake. Kisha Yesu akamwambia, “Hakikisha humwambii mtu yeyote. Lakini nenda ukajionyeshe kwa kuhani, na utoe sadaka aliyoamuru Mose, ili kuwa ushuhuda kwao.”

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mathayo 8:1-4