Malaki Utangulizi
Utangulizi
Maana ya jina Malaki ni “Mjumbe Wangu” au “Mjumbe wa Mwenyezi Mungu”. Malaki aliishi baada ya Hekalu la pili kujengwa. Maisha ya uchaji wa Mwenyezi Mungu ya Wayahudi yalikuwa mabaya: Walikuwa wamekengeuka, wakawaoa wanawake wa mataifa mengine, na wakaacha kutoa zaka na dhabihu kwa Mwenyezi Mungu. Habari hizi zinafanana sana na mwisho wa kitabu cha Nehemia, ambaye kuna uwezekano mkubwa aliishi wakati mmoja na Malaki.
Mwandishi
Malaki.
Kusudi
Kuwahimiza watu wafanye mabadiliko thabiti ya kimsingi katika maisha yao kwa kuziacha dhambi zao ili kurejesha uhusiano wao na Mwenyezi Mungu, na kuwakumbusha kuhusu upendo wa Mwenyezi Mungu.
Mahali
Yerusalemu na Hekaluni.
Tarehe
Mnamo 430 K.K.
Wahusika Wakuu
Malaki, makuhani, na watu wa Yuda.
Wazo Kuu
Upendo wa Mwenyezi Mungu hauna kikomo wala mipaka.
Mambo Muhimu
Kitabu hiki kinaonesha kuwa Hekalu lilijengwa tena, na dhabihu na sikukuu zikarudishwa. Ufahamu wa jumla wa Torati ulirudishwa tena na Ezra, na kurudi kwao nyuma kimaadili kulikofuatia kulitokea zaidi miongoni mwa makuhani.
Yaliyomo
Upendo wa Mwenyezi Mungu kwa Israeli (1:1-5)
Israeli wamtukana Mwenyezi Mungu (1:6–2:16)
Hukumu ya Mwenyezi Mungu na ahadi yake (2:17–4:6).
Iliyochaguliwa sasa
Malaki Utangulizi: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
![None](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2F58%2Fhttps%3A%2F%2Fweb-assets.youversion.com%2Fapp-icons%2Fsw.png&w=128&q=75)
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.