Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka 11:1-4

Luka 11:1-4 NEN

Siku moja, Yesu alikuwa mahali fulani akiomba. Alipomaliza kuomba, mmoja wa wanafunzi wake akamwambia, “Bwana, tufundishe kuomba, kama vile Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake.” Akawaambia, “Mnapoomba, semeni: “ ‘Baba yetu (uliye mbinguni), jina lako litukuzwe, ufalme wako uje. (Mapenzi yako yafanyike hapa duniani kama huko mbinguni.) Utupatie kila siku riziki yetu. Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa na sisi huwasamehe wote wanaotukosea. Wala usitutie majaribuni (bali utuokoe kutoka kwa yule mwovu).’ ”

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Luka 11:1-4