Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Walawi 24:1-9

Walawi 24:1-9 NEN

BWANA akamwambia Mose, “Waagize Waisraeli wakuletee mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa kwa ajili ya mwanga ili taa ziwe zinawaka daima. Nje ya pazia la Ushuhuda ndani ya Hema la Kukutania, Aroni ataziwasha taa mbele za BWANA kuanzia jioni hadi asubuhi bila kuzima. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo. Taa zilizo juu ya kinara cha dhahabu safi mbele za BWANA lazima zihudumiwe daima. “Chukua unga laini, uoke mikate kumi na miwili, ukitumia sehemu mbili za kumi za efa za unga kwa kila mkate. Iweke katika mistari miwili, kila mstari mikate sita, uiweke mbele za BWANA juu ya meza iliyotengenezwa kwa dhahabu safi. Kando ya kila mstari, weka uvumba safi kama sehemu ya kumbukumbu ili kuwakilisha mikate kuwa sadaka iliyotolewa kwa BWANA kwa kuteketezwa kwa moto. Mikate hii itawekwa mbele za BWANA kila wakati, Sabato baada ya Sabato, kwa niaba ya Waisraeli, kuwa Agano la kudumu. Hii ni mali ya Aroni na wanawe, watakaoila katika mahali patakatifu, kwa sababu ni sehemu takatifu sana ya fungu lao la kawaida la sadaka iliyotolewa kwa BWANA kwa kuteketezwa kwa moto.”