Yuda Utangulizi
Utangulizi
Mwandishi wa waraka huu ni Yuda, aliyekuwa nduguye Yesu na Yakobo, yule aliyekuwa msimamizi wa Baraza la Yerusalemu, na mwandishi wa waraka wa Yakobo.
Muktadha wa waraka huu na yale yaliyomo kwenye waraka wa 2 Petro yanaashiria kuwa Yuda alikuwa amehamasishwa na ujumbe wa Petro. Yuda anaonesha kuwa alikusudia kuandika kuhusu wokovu, lakini akabadili nasaha zake ili kukemea mtazamo wa watu fulani wenye tabia mbaya, waliokuwa wakizunguka miongoni mwa waumini wakipotosha neema ya Mungu.
Mwandishi
Yuda, ndugu yake Yesu.
Kusudi
Kukumbusha kanisa umuhimu wa kuitetea imani, na kulionya juu ya watu waovu wanaozunguka miongoni mwao wakipotosha imani.
Mahali
Hapajulikani.
Tarehe
Mnamo 65 B.K.
Wahusika Wakuu
Yuda, Yakobo, na Yesu.
Wazo Kuu
Yuda anasisitiza umuhimu wa kuitetea imani. Wapotovu na wazushi ni lazima waoneshwe wazi kwamba sio wa kweli. Yuda anaonya kwamba hukumu ya Mungu itawafikia wale waliopotoka katika imani, kama vile ilivyowafikia Kaini, Kora, na Balaamu.
Mambo Muhimu
Kuweka wazi walimu wa uongo na kuwakemea vikali. Anamalizia ujumbe wake kwa kuonesha wazi kwamba Mungu anaweza kumlinda muumini, ili aweze kuishi maisha yaliyonyooka, na hatimaye kufika mbele ya Mungu bila lawama wala mawaa.
Yaliyomo
Salamu na utangulizi (1‑4)
Hukumu kwa walimu wa uongo (5‑16)
Adibisho na hitimisho (17‑25).
Iliyochaguliwa sasa
Yuda Utangulizi: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Biblia Takatifu™ Neno™
Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Version™
Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.