Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yuda 1:17-25

Yuda 1:17-25 NENO

Lakini ninyi wapendwa, kumbukeni yale mitume wa Bwana wetu Isa Al-Masihi waliyotabiri awali. Kwa kuwa waliwaambia, “Siku za mwisho kutakuwa na watu wenye kudhihaki, watakaofuata tamaa zao wenyewe za upotovu.” Hawa ndio watu wanaowagawanya ninyi, wanaofuata tamaa zao za asili, wala hawana Roho wa Mungu. Lakini ninyi wapendwa, jijengeni katika imani yenu iliyo takatifu sana tena ombeni katika Roho wa Mungu. Jilindeni katika upendo wa Mungu mkitazamia rehema ya Bwana wetu Isa Al-Masihi, inayowapeleka katika uzima wa milele. Wahurumieni walio na mashaka; okoeni wengine kwa kuwanyakua kutoka motoni; nao wengine wahurumieni mkiwa na hofu, mkichukia hata vazi lenye mawaa na kutiwa unajisi na mwili. Kwake yeye awezaye kuwalinda ninyi msianguke na kuwaleta mbele za utukufu wake mkuu bila dosari na kwa furaha ipitayo kiasi: kwake yeye Mungu pekee Mwokozi wetu, kwa Isa Al-Masihi Bwana wetu, utukufu, ukuu, uweza na mamlaka ni vyake tangu milele, sasa na hata milele! Amen.