Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yeremia 7:1-11

Yeremia 7:1-11 NENO

Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Mwenyezi Mungu: “Simama kwenye lango la nyumba ya Mwenyezi Mungu, na huko upige mbiu ya ujumbe huu: “ ‘Sikieni neno la Mwenyezi Mungu, enyi watu wote wa Yuda mliokuja kupitia malango haya ili kumwabudu Mwenyezi Mungu. Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli: Tengenezeni njia zenu na matendo yenu, nami nitawaacha mkae mahali hapa. Msitumainie maneno ya udanganyifu na kusema, “Hili ni Hekalu la Mwenyezi Mungu, Hekalu la Mwenyezi Mungu, Hekalu la Mwenyezi Mungu!” Kama kweli mkibadili njia zenu na matendo yenu, mkatendeana haki kila mmoja na mwenzake, kama hamdhulumu mgeni, yatima wala mjane, na kumwaga damu isiyo na hatia mahali hapa, nanyi kama hamtafuata miungu mingine kwa madhara yenu wenyewe, ndipo nitawaacha mkae mahali hapa, katika nchi niliyowapa baba zenu milele na milele. Lakini tazama, mnatumainia maneno ya udanganyifu yasiyo na maana. “ ‘Je, mtaiba na kuua, mtazini na kuapa kwa uongo, na kufukiza uvumba kwa Baali, na kufuata miungu mingine ambayo hamkuijua, kisha mje na kusimama mbele yangu katika nyumba hii inayoitwa kwa Jina langu, mkisema, “Tuko salama.” Salama kwa kufanya mambo haya yote ya kuchukiza? Je, nyumba hii, iitwayo kwa Jina langu, imekuwa pango la wanyang’anyi kwenu? Lakini nimekuwa nikiona yanayotendeka! asema Mwenyezi Mungu.