Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yeremia 1:9-14

Yeremia 1:9-14 NENO

Kisha Mwenyezi Mungu akaunyoosha mkono wake na kugusa kinywa changu, akaniambia, “Sasa nimeyaweka maneno yangu kinywani mwako. Tazama, leo nimekuweka juu ya mataifa na falme ili kung’oa na kubomoa, kuharibu na kuangamiza, kujenga na kupanda.” Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema, “Je, Yeremia unaona nini?” Nami nikajibu, “Naona tawi la mti wa mlozi.” Mwenyezi Mungu akaniambia, “Umeona vyema kwa maana ninaliangalia neno langu ili kuona kwamba limetimizwa.” Neno la Mwenyezi Mungu likanijia tena, “Unaona nini?” Nikajibu, “Naona chungu kinachochemka, kikiwa kimeinama kutoka kaskazini.” Mwenyezi Mungu akaniambia, “Kutoka kaskazini maafa yatamwagwa kwa wote wanaoishi katika nchi.