Yeremia 1:9-14
Yeremia 1:9-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha Mwenyezi-Mungu akaunyosha mkono wake, akagusa kinywa changu, akaniambia, “Tazama nimeyatia maneno yangu kinywani mwako. Leo nimekupa mamlaka juu ya mataifa na falme, uwe na mamlaka ya kungoa na kubomoa, mamlaka ya kuharibu na kuangamiza, mamlaka ya kujenga na ya kupanda.” Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia: “Yeremia, unaona nini?” Nami nikasema, “Ninaona tawi la mlozi unaochanua.” Mwenyezi-Mungu akaniambia, “Umeona vizuri, maana niko macho kulitekeleza neno langu.” Neno la Mwenyezi-Mungu likanijia mara ya pili: “Unaona nini?” Nami nikasema, “Ninaona chungu kinatokota kimeinama upande wangu kutoka kaskazini.” Mwenyezi-Mungu akaniambia, “Maangamizi yataanzia kutoka kaskazini na kuwapata wakazi wote wa nchi hii.
Yeremia 1:9-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo BWANA akaunyosha mkono wake, akanigusa kinywa changu; BWANA akaniambia, Tazama, nimetia maneno yangu kinywani mwako; angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda. Tena neno la BWANA likanijia, kusema, Yeremia, waona nini? Nikasema, Naona ufito wa mlozi. Ndipo BWANA akaniambia, Umeona vema, kwa maana ninaliangalia neno langu, ili nilitimize. Neno la BWANA likanijia mara ya pili, kusema, Waona nini? Nikasema, Naona sufuria lenye maji yatokotayo, na mdomo wake unaelekea toka upande wa kaskazini. Ndipo BWANA akaniambia, Toka kaskazini mabaya yatatokea, na kuwapata watu wote wakaao katika nchi hii.
Yeremia 1:9-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ndipo BWANA akaunyosha mkono wake, akanigusa kinywa changu; BWANA akaniambia, Tazama, nimetia maneno yangu kinywani mwako; angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung’oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda. Tena neno la BWANA likanijia, kusema, Yeremia, waona nini? Nikasema, Naona ufito wa mlozi. Ndipo BWANA akaniambia, Umeona vema, kwa maana ninaliangalia neno langu, ili nilitimize. Neno la BWANA likanijia mara ya pili, kusema, Waona nini? Nikasema, Naona sufuria lenye maji yatokotayo, na mdomo wake unaelekea toka upande wa kaskazini. Ndipo BWANA akaniambia, Toka kaskazini mabaya yatatokea, na kuwapata watu wote wakaao katika nchi hii.
Yeremia 1:9-14 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Kisha Mwenyezi Mungu akaunyoosha mkono wake na kugusa kinywa changu, akaniambia, “Sasa nimeyaweka maneno yangu kinywani mwako. Tazama, leo nimekuweka juu ya mataifa na falme ili kung’oa na kubomoa, kuharibu na kuangamiza, kujenga na kupanda.” Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema, “Je, Yeremia unaona nini?” Nami nikajibu, “Naona tawi la mti wa mlozi.” Mwenyezi Mungu akaniambia, “Umeona vyema kwa maana ninaliangalia neno langu ili kuona kwamba limetimizwa.” Neno la Mwenyezi Mungu likanijia tena, “Unaona nini?” Nikajibu, “Naona chungu kinachochemka, kikiwa kimeinama kutoka kaskazini.” Mwenyezi Mungu akaniambia, “Kutoka kaskazini maafa yatamwagwa kwa wote wanaoishi katika nchi.