Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 62:6-12

Isaya 62:6-12 NEN

Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, ee Yerusalemu, hawatanyamaza mchana wala usiku. Ninyi wenye kumwita BWANA, msitulie, msimwache apumzike hadi atakapoufanya imara Yerusalemu na kuufanya uwe sifa ya dunia. BWANA ameapa kwa mkono wake wa kuume na kwa mkono wake wenye nguvu: “Kamwe sitawapa tena adui zenu nafaka zenu kama chakula chao; kamwe wageni hawatakunywa tena divai mpya ambayo mmeitaabikia, lakini wale waivunao nafaka wataila na kumsifu BWANA, nao wale wakusanyao zabibu watainywa divai yake katika nyua za patakatifu pangu.” Piteni, piteni katika malango! Tengenezeni njia kwa ajili ya watu. Jengeni, jengeni njia kuu! Ondoeni mawe. Inueni bendera kwa ajili ya mataifa. BWANA ametoa tangazo mpaka miisho ya dunia: “Mwambie Binti Sayuni, ‘Tazama, mwokozi wako anakuja! Tazama ujira wake uko pamoja naye, na malipo yake yanafuatana naye!’ ” Wataitwa Watu Watakatifu, Waliokombolewa na BWANA; nawe utaitwa Aliyetafutwa, Mji Usioachwa Tena.