Isaya 62:1-5
Isaya 62:1-5 NENO
Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, hadi haki yake itakapoangaza kama mapambazuko, wokovu wake kama mwanga wa moto. Mataifa wataona haki yako, nao wafalme wote wataona utukufu wako; wewe utaitwa kwa jina jipya lile ambalo kinywa cha Mwenyezi Mungu kitatamka. Utakuwa taji la fahari mkononi mwa Mwenyezi Mungu, taji la kifalme mkononi mwa Mungu wako. Hawatakuita tena Aliyeachwa, wala nchi yako kuiita Ukiwa. Bali utaitwa Hefsiba, nayo nchi yako itaitwa Beula, kwa maana Mwenyezi Mungu atakufurahia, nayo nchi yako itaolewa. Kama vile kijana aoavyo mwanamwali, ndivyo Mwashi wako atakavyokuoa; kama bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi wake, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe.