Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 18

18
Unabii dhidi ya Kushi
1Ole kwa nchi ya mvumo wa mabawa#18:1 au wa nzige,
kando ya mito ya Kushi,
2iwapelekayo wajumbe wake kupitia bahari
kwa mashua za mafunjo juu ya maji.
Nendeni, wajumbe wepesi,
kwa taifa la watu warefu wenye ngozi nyororo,
kwa taifa linaloogopwa mbali na karibu,
taifa gomvi lenye lugha ngeni,
ambalo nchi yao imegawanywa kwa mito.
3Enyi mataifa yote ya ulimwengu,
ninyi mnaoishi duniani
wakati bendera itakapoinuliwa milimani,
mtaiona,
nayo tarumbeta itakapolia,
mtaisikia.
4Hili ndilo Mwenyezi Mungu aliloniambia:
“Nitatulia kimya na kutazama
kutoka maskani yangu,
kama joto linalometameta katika mwanga wa jua,
kama wingu la umande
katika joto la wakati wa mavuno.”
5Kwa maana, kabla ya mavuno,
wakati wa kuchanua ukishapita
na maua yakawa zabibu zinazoiva,
atayakata machipukizi kwa mundu wa kupogolea matawi,
naye atakata na kuyaondoa matawi yaliyopanuka.
6Yote yataachwa kwa ajili ya ndege wawindao wa mlimani
na wanyama pori,
ndege watajilisha juu yake wakati wote wa kiangazi,
nao wanyama pori wakati wote wa masika.
7Wakati huo matoleo yataletwa kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni
kutoka kwa taifa la watu warefu wenye ngozi nyororo,
kutoka kwa taifa linaloogopwa mbali na karibu,
kutoka taifa gomvi lenye lugha ngeni,
ambalo nchi yao imegawanywa kwa mito,
matoleo yataletwa katika Mlima Sayuni, mahali pa Jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.

Iliyochaguliwa sasa

Isaya 18: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia