Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waebrania 7:4-10

Waebrania 7:4-10 NENO

Tazama jinsi alivyokuwa mkuu: Hata Ibrahimu, baba yetu wa zamani, alimpa sehemu ya kumi ya nyara zake. Basi sheria inawaagiza wana wa Lawi ambao hufanyika makuhani kupokea sehemu ya kumi kutoka kwa watu ambao ni ndugu zao, ingawa ndugu zao ni wazao wa Ibrahimu. Huyu Melkizedeki, ingawa hakufuatia ukoo wake kutoka kwa Lawi, lakini alipokea sehemu ya kumi kutoka kwa Ibrahimu na kumbariki yeye aliyekuwa na zile ahadi. Wala hakuna shaka kwamba mdogo hubarikiwa na aliye mkuu kuliko yeye. Kwa upande mmoja, sehemu ya kumi hupokelewa na watu ambao hufa; lakini kwa upande mwingine hupokelewa na yeye ambaye hushuhudiwa kuwa yu hai. Mtu anaweza hata kusema kwamba Lawi, ambaye hupokea sehemu ya kumi, alitoa hiyo sehemu ya kumi kupitia kwa Ibrahimu, kwa sababu Melkizedeki alipokutana na Ibrahimu, Lawi alikuwa bado katika viuno vya baba yake wa zamani.