Waebrania 4:8-13
Waebrania 4:8-13 NENO
Kwa maana kama Yoshua angelikuwa amewapa raha, Mungu hangesema tena baadaye kuhusu siku nyingine. Basi, imebaki raha ya Sabato kwa ajili ya watu wa Mungu; kwa kuwa kila mmoja aingiaye katika raha ya Mungu pia hupumzika kutoka kazi zake mwenyewe, kama vile Mungu alivyopumzika kutoka kazi zake. Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha hiyo, ili asiwepo yeyote atakayeanguka kwa kufuata mfano wao wa kutokutii. Kwa maana neno la Mungu li hai tena lina nguvu. Lina makali kuliko upanga wowote wenye makali kuwili, hivyo linachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, viungo na mafuta yaliyo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Wala hakuna kiumbe chochote kilichofichika machoni pa Mungu. Kila kitu kimefunuliwa na kiko wazi machoni pake yeye ambaye lazima tutawajibika kwake.