Waebrania 4:8-13
Waebrania 4:8-13 Biblia Habari Njema (BHN)
Kama Yoshua angekuwa amewapa watu hao hilo pumziko, Mungu hangalisema baadaye juu ya siku nyingine. Kwa hiyo, basi, bado kuna kupumzika kwa watu wa Mungu. Maana, kila aingiaye mahali pa pumziko la Mungu atapumzika kutoka katika kazi yake kama vile pia Mungu alivyopumzika kutoka kazi yake. Basi, tujitahidi kuingia katika pumziko hilo, ili asiwepo yeyote miongoni mwetu atakayekataa kutii kama walivyofanya wao. Neno la Mungu ni hai na lina nguvu; ni kali kuliko upanga wenye makali kuwili. Hukata kabisa mpaka mahali ambapo moyo na roho hukutana, mpaka pale vikutanapo viungo vya mwili na uboho. Neno hilo huchambua nia na fikira za mioyo ya watu. Hakuna kiumbe chochote kilichofichika mbele ya Mungu; kila kitu kimefunuliwa wazi mbele ya macho yake yeye ambaye kwake tutapaswa kutoa hoja ya matendo yetu.

Waebrania 4:8-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana kama Yoshua angaliwapa pumziko, asingaliinena siku nyingine baadaye. Basi, limesalia pumziko la sabato kwa watu wa Mungu. Kwa maana yeye aliyeingia katika pumziko lake amepumzika mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyopumzika katika kazi zake. Basi, na tufanye bidii kuingia katika pumziko lile, ili kwamba mtu yeyote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa kuasi. Maana neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena ni jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, maana vitu vyote ni tupu na kuwekwa wazi machoni pake yeye ambaye tunapaswa kuwajibika kwake.
Waebrania 4:8-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maana kama Yoshua angaliwapa raha, asingaliinena siku nyingine baadaye. Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu. Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake amestarehe mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake. Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha ile, ili kwamba mtu ye yote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa kuasi. Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu.
Waebrania 4:8-13 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Kwa maana kama Yoshua angelikuwa amewapa raha, Mungu hangesema tena baadaye kuhusu siku nyingine. Basi, imebaki raha ya Sabato kwa ajili ya watu wa Mungu; kwa kuwa kila mmoja aingiaye katika raha ya Mungu pia hupumzika kutoka kazi zake mwenyewe, kama vile Mungu alivyopumzika kutoka kazi zake. Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha hiyo, ili asiwepo yeyote atakayeanguka kwa kufuata mfano wao wa kutokutii. Kwa maana neno la Mungu li hai tena lina nguvu. Lina makali kuliko upanga wowote wenye makali kuwili, hivyo linachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, viungo na mafuta yaliyo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Wala hakuna kiumbe chochote kilichofichika machoni pa Mungu. Kila kitu kimefunuliwa na kiko wazi machoni pake yeye ambaye lazima tutawajibika kwake.