Mwanzo 5:1-5
Mwanzo 5:1-5 NENO
Hii ni orodha iliyoandikwa ya vizazi vya Adamu. Mungu alipomuumba mwanadamu, alimfanya kwa sura ya Mungu. Aliwaumba mwanaume na mwanamke, akawabariki. Walipokwisha kuumbwa, akawaita “Binadamu.” Adamu alipokuwa ameishi miaka mia moja na thelathini, alimzaa mwana aliyekuwa na sura yake, mwenye kufanana naye. Akamwita jina Sethi. Baada ya Sethi kuzaliwa, Adamu aliishi miaka mia nane, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. Adamu aliishi jumla ya miaka mia tisa na thelathini, ndipo akafa.