Mwanzo 5:1-5
Mwanzo 5:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Ifuatayo ni orodha ya wazawa wa Adamu. Wakati Mungu alipomuumba binadamu, alimuumba kwa mfano wake. Aliwaumba mwanamume na mwanamke, kisha akawabariki na kuwapa jina “Binadamu.” Adamu alipokuwa na umri wa miaka 130, alipata mtoto aliyefanana naye, na mwenye sura kama yake; akamwita Sethi. Baada ya kumzaa Sethi, Adamu aliishi miaka 800, na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Adamu alifariki akiwa na umri wa miaka 930.
Mwanzo 5:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya; mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa. Adamu akaishi miaka mia moja na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi. Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia tisa na thelathini, naye akafa.
Mwanzo 5:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya; mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa. Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi. Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake. Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa.
Mwanzo 5:1-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Hii ni orodha iliyoandikwa ya vizazi vya Adamu. Mungu alipomuumba mwanadamu, alimfanya kwa sura ya Mungu. Aliwaumba mwanaume na mwanamke, akawabariki. Walipokwisha kuumbwa, akawaita “Binadamu.” Adamu alipokuwa ameishi miaka mia moja na thelathini, alimzaa mwana aliyekuwa na sura yake, mwenye kufanana naye. Akamwita jina Sethi. Baada ya Sethi kuzaliwa, Adamu aliishi miaka mia nane, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. Adamu aliishi jumla ya miaka mia tisa na thelathini, ndipo akafa.