Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 49:1-12

Mwanzo 49:1-12 NEN

Ndipo Yakobo akawaita wanawe na kusema: “Kusanyikeni kunizunguka ili niweze kuwaambia lile litakalowatokea siku zijazo. “Kusanyikeni na msikilize, enyi wana wa Yakobo, msikilizeni baba yenu Israeli. “Reubeni, wewe ni mzaliwa wangu wa kwanza, nguvu zangu, tunda la kwanza la nguvu zangu, umepita kwa heshima, umepita kwa uwezo. Usiyezuiwa kama maji, basi hutakuwa mkuu tena, kwa kuwa ulipanda kwenye kitanda cha baba yako, kwenye kitanda changu na kukinajisi. “Simeoni na Lawi ni wana ndugu: panga zao ni silaha za jeuri. Mimi na nisiingie katika baraza lao, nami nisiunganike katika kusanyiko lao, kwa kuwa wamewaua watu katika hasira yao, walikata mishipa ya miguu ya mafahali kama walivyopenda. Hasira yao na ilaaniwe, kwa kuwa ni kali mno, nayo ghadhabu yao ni ya ukatili! Nitawatawanya katika Yakobo Na kuwasambaza katika Israeli. “Yuda, ndugu zako watakusifu; mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako; wana wa baba yako watakusujudia. Ee Yuda, wewe ni mwana simba; unarudi toka mawindoni, mwanangu. Kama simba hunyemelea na kulala chini, kama simba jike: nani athubutuye kumwamsha? Fimbo ya ufalme haitaondoka kwa Yuda, wala fimbo ya mtawala kati ya miguu yake, hadi aje yeye ambaye milki ni yake, ambaye utii wa mataifa ni wake. Atamfunga punda wake katika mzabibu, naye mwana-punda wake kwenye tawi lililo bora zaidi; atafua mavazi yake katika divai, majoho yake katika damu ya mizabibu. Macho yake yatakuwa mekundu kwa divai, meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mwanzo 49:1-12