Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 49:1-12

Mwanzo 49:1-12 Biblia Habari Njema (BHN)

Yakobo akawaita wanawe, akasema, “Kusanyikeni pamoja niwaambieni mambo yatakayowapata siku zijazo. “Kusanyikeni msikie, enyi wana wa Yakobo, nisikilizeni mimi Israeli, baba yenu. “Wewe Reubeni ni mzaliwa wangu wa kwanza, nguvu yangu na tunda la ujana wangu. Wewe wawapita ndugu zako kwa ukuu na nguvu. “Wewe ni kama maji ya mafuriko. Lakini hutakuwa wa kwanza tena, maana ulipanda kitandani mwangu mimi baba yako, wewe ulikitia najisi; naam wewe ulikipanda! “Simeoni na Lawi ni ndugu: Silaha zao wanatumia kufanya ukatili, lakini mimi sitashiriki njama zao; ee roho yangu, usishiriki mikutano yao, maana, katika hasira yao, walimuua mtu, kwa utundu wao walikata mshipa wa ng'ombe. “Nalaani hasira yao maana ni kali mno, na ghadhabu yao isiyo na huruma. Nitawatawanya katika nchi ya Yakobo, nitawasambaza katika nchi ya Israeli. “Wewe Yuda, ndugu zako watakusifu. Adui zako utawakaba shingo; na ndugu zako watainama mbele yako. “Wewe Yuda, mwanangu, ni kama mwanasimba ambaye amepata mawindo yake akapanda juu. Kama simba hujinyosha na kulala chini; simba mwenye nguvu, nani athubutuye kumwamsha? “Fimbo ya kifalme haitatoka kwa Yuda, wala bakora ya utawala miguuni pake, mpaka atakapofika yule ambaye ni yake; ambaye mataifa yatamtii. “Atafunga punda wake katika mzabibu na mwanapunda wake kwenye mzabibu bora. Hufua nguo zake katika divai, na mavazi yake katika divai nyekundu. “Macho yake ni mekundu kwa divai, meno yake ni meupe kwa maziwa.

Shirikisha
Soma Mwanzo 49

Mwanzo 49:1-12 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)

Ndipo Yakobo akawaita wanawe na kusema: “Kusanyikeni kunizunguka ili niweze kuwaambia lile litakalowatokea siku zijazo. “Kusanyikeni na msikilize, enyi wana wa Yakobo, msikilizeni baba yenu Israeli. “Reubeni, wewe ni mzaliwa wangu wa kwanza, nguvu zangu, tunda la kwanza la nguvu zangu, umepita kwa heshima, umepita kwa uwezo. Usiyezuiwa kama maji, basi hutakuwa mkuu tena, kwa kuwa ulipanda kwenye kitanda cha baba yako, kwenye kitanda changu na kukinajisi. “Simeoni na Lawi ni wana ndugu: panga zao ni silaha za jeuri. Mimi na nisiingie katika baraza lao, nami nisiunganike katika kusanyiko lao, kwa kuwa wamewaua watu katika hasira yao, walikata mishipa ya miguu ya mafahali kama walivyopenda. Hasira yao na ilaaniwe, kwa kuwa ni kali mno, nayo ghadhabu yao ni ya ukatili! Nitawatawanya katika Yakobo Na kuwasambaza katika Israeli. “Yuda, ndugu zako watakusifu; mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako; wana wa baba yako watakusujudia. Ee Yuda, wewe ni mwana simba; unarudi toka mawindoni, mwanangu. Kama simba hunyemelea na kulala chini, kama simba jike: nani athubutuye kumwamsha? Fimbo ya ufalme haitaondoka kwa Yuda, wala fimbo ya mtawala kati ya miguu yake, hadi aje yeye ambaye milki ni yake, ambaye utii wa mataifa ni wake. Atamfunga punda wake katika mzabibu, naye mwana-punda wake kwenye tawi lililo bora zaidi; atafua mavazi yake katika divai, majoho yake katika damu ya mizabibu. Macho yake yatakuwa mekundu kwa divai, meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa.

Shirikisha
Soma Mwanzo 49