Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 19:30-38

Mwanzo 19:30-38 NENO

Lutu na binti zake wawili waliondoka Soari na kufanya makao yao kule milimani, kwa maana aliogopa kukaa Soari. Yeye na binti zake wawili waliishi katika pango. Siku moja binti mkubwa akamwambia yule mdogo, “Baba yetu ni mzee, na hakuna mwanaume mahali hapa atakayekutana na sisi kimwili, kama ilivyo desturi ya mahali pote duniani. Tumnyweshe baba yetu mvinyo, kisha tukutane naye kimwili ili tuhifadhi uzao wetu kupitia baba yetu.” Usiku ule walimnywesha baba yao mvinyo; alipolewa, binti yake mkubwa akaingia na kukutana naye kimwili. Baba yao hakujua binti yake alipoingia kulala naye wala alipotoka. Siku iliyofuata binti mkubwa akamwambia yule mdogo, “Usiku uliopita mimi nilikutana kimwili na baba yangu. Tumnyweshe divai tena, usiku huu nawe ukutane naye kimwili ili tuweze kuhifadhi uzao wetu kupitia baba yetu.” Kwa hiyo wakamnywesha baba yao mvinyo tena usiku ule, naye binti yake mdogo akaingia, akakutana naye kimwili. Kwa mara nyingine baba yao hakujua binti yake alipolala naye wala alipoondoka. Hivyo binti wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao. Binti mkubwa akamzaa mwana, akamwita jina Moabu; ndiye baba wa Wamoabu hata leo. Binti mdogo pia akamzaa mwana, naye akamwita jina Benami; ndiye baba wa Waamoni hata leo.